SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUFUFUA SKIMU YA MATIPWILI

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema iko tayari kufufua na kuboresha skimu ya Umwagiliaji Matipwili iliyopo Kata ya Mkangwe, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamebainika kufuatia mafunzo ya usimamizi, uendeshaji na matunzo ya miundombinu ya Umwagiliaji yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, yakilenga kuongeza tija na kufufua matumizi ya eneo la zaidi ya ekari 500 zinazofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Salome Njau, amesema Serikali ipo tayari kuboresha na kufufua skimu hiyo ili iweze kutumika kikamilifu, akibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa zaidi ya wakulima 2,570, ni wachache tu wanaotumia eneo hilo kutokana na kutegemea mvua.

Amesisitiza umuhimu wa usajili wa chama cha Umwagiliaji na wakulima kuingizwa kwenye mfumo wa kitaifa (IMIS) ili kurahisisha utoaji wa huduma na usimamizi bora.

Kwa upande wake, Mhandisi wa Umwagiliaji Wilaya ya Bagamoyo, Anselmo Mkanuwoga, amesema mafunzo hayo yatawajengea wakulima uwezo wa kuongoza vyama vyao pamoja na kutunza miundombinu ya skimu, jambo litakalosaidia mradi kudumu kwa muda mrefu na kuongeza uzalishaji.

Ameongeza kuwa wakulima watakapozalisha kwa tija, itakuwa rahisi kwao kuchangia ada za huduma ya Umwagiliaji, hatua muhimu kwa uendelevu wa skimu.

Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bi. Pendo Sanga, amesema mafunzo hayo muhimu yatawajengea wakulima uelewa wa majukumu yao pamoja na kuhimiza usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji, ulipaji wa ada za Umwagiliaji na matumizi sahihi ya miundombinu ili kuongeza tija na kupata masoko ya uhakika.

Naye mkulima wa skimu hiyo, Leticia Mdoe, amesema mafunzo hayo yamefungua uelewa mpya kwa wakulima na kuwapa wajibu wa kutunza miundombinu kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.

Ameeleza kuwa elimu waliyoipata itawawezesha kuongeza uzalishaji, kipato na kuweza kuwasilisha malalamiko na mapendekezo moja kwa moja tume kwa njia ya mtandao na kuboresha maisha ya familia zao kupitia kilimo chenye tija.

Mafunzo hayo yanatajwa kuwa mwanzo wa safari mpya ya maendeleo katika Skimu ya Matipwili, ambapo kupitia ushirikiano huu.

spot_img

Latest articles

Tanzania, AngloGold Ashanti kuimarisha ushirikiano

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa kampuni ya...

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...

More like this

Tanzania, AngloGold Ashanti kuimarisha ushirikiano

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa kampuni ya...

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...