Nderiananga akemea unyanyapaa kwa watu wanaoshi na VVU

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amekemea vitendo vya unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (WAVIU) na kuiasa jamii kuendelea kuwajali na kuwajumuisha katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu kuhusu masuala ya UKIMWI katika mkoa wake, wakati alipomtembelea ofisi kwake Kilimanjaro Julai 17, 2023.

Ametoa kauli hiyo Julai 17, 2023 wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli za WAVIU, katika Konga za watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika Wilaya za Moshi ambapo alifanikiwa kuzungumza nao na kukagua shughuli za uzalishaji wanazofanya.

Ummy aliitaka jamii kutowanyanyapaa watu wanaoishi na VVU na kuwashirikisha katika shughuli za kijamii na za uzalishaji mali, huku akieleza kuwa ni watu muhimu na wenye mchango chanya kwenye kujiletea maendeleo yao na Taifa.

“Tuache unyanyapaa kwa WAVIU, tusiwabague, tuishi nao kama watu wengine, tuwapende na tujenge tabia ya kuwathamini, kujali na kuwajumuisha katika masuala mbalimbali ya uzalishaji huku tukiunga mkono jitihada za Serikali za kupinga unyanyapaa huo,” alisema Mhe. Nderiananga

Aidha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha vijana wanaoishi na maambukizi ya VVU kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri zao kujiongezea mitaji na kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na vikundi vya uzalishaji mali huku akiwakumbusha kuendelea kujali afya zao kwa kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI.

“Kwa tunaoendelea kutumia dawa za ARVs niwasihii sana tusiache wala kuzipuuza, tumeona zinasaidia wengi na nitoe rai kwa kila anayegundulika na maambuki ya Virusi vya UKIMWI, basi ni vyema aanze dawa hizi mapema ili aweze kuishi katika hali bora zaidi,” alisisitiza

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu alitumia nafasi yake kukumbusha vijana kujitokeza kwa wingi kupima na kujua hali zao huku akiwakumbusha kuwa ndilo kundi linaloathiriwa zaidi na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

“Pamoja na jitihada za Serikali katika mapambano haya, bado vijana mnakazi kubwa ya kuendelea kujilinda kwa njia zote muhimu zinazoshauriwa na wataalam wa afya huku mkikumbuka kuachana na tabia zote hatarishi zinazoweza kuchochea mtu kupata maambukizi haya,”alieleza Babu.

Awali akitoa taarifa fupi ya hali ya UKIMWI kwa Mkoa wa Kilimanjaro, mratibu wa masuala ya UKIMWI Mtambuka, Jesca Nyaki alisema kiwango cha maambukizi kimeendelea kupungua kwa kuzingatia takwimu zilizopo, ambapo kimepungua kutoka asilimia 7.3 kwa mwaka 2003/24 hadi asilimia 2.6 mwaka 2016/17.

Mwenyekiti wa Konga ya Moshi Vijijini, Baltazar Minishi ameishukuru Serikali kwa uwezeshwaji na huduma za afya wanazozipata kutoka serikalini kwani zimeboreshwa na kuleta tija kwa WAVIU.

Aidha, Baltazar Munishi ameomba serikali iwapatie Ofisi kwa ajili ya Utekelezaji wa shughuli zao,ambapo Mkurugenzi wa Halmashuri ya Moshi, Shadrack Muhagama ameahidi kutatua changamoto hiyo na kuwapatia Ofisi kwa kadri itakavyowezekana.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...