Yanga yakomaa kileleni, Simba yavizia ikitafuna  miwa Morogoro

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI Yanga wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo baada ya   ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Bacca dk 41, Laurindo Depu dk 73, Pacome  Zouzoua dk 81. Wanajangwani hao wamefikisha alama 69 katika michezo 28 waliyocheza na kuendelea  kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Katika mchezo mwingine, Mnyama Simba ameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa  Jamhuri, Morogoro huku akiendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi   akiwa na alama 67 baada ya mechi 28.

Wafungaji wa Simba ni Rushine de Reuck dk 9’p, Selemani  Mwalimu dk 77’, Anicent Oura dk 90.

Mechi zilizobaki kwa vigogo hao wa Kariakoo, Yanga itacheza na TRA United nyumbani, kisha JKT Tanzania. Simba itakutana na Singida Bs na KMC, itakuwa nyumbani mechi zote.

Matokeo mengine ya mechi za raundi ya 28

 FT: Singida BS 3-1 TZ Prisons (Mossi 2’, 61’, Kennedy 23’ / Sengati 49’)
FT: TRA United 1-1 Coastal Union (Kombo 54’p / Maabad 68’p)
FT: Dodoma Jiji 0-0 JKT Tanzania
FT: Pamba Jiji 0-2 Mbeya City (Ambokile 18’, 76’)
FT: Fountain Gate 0-1 Mashujaa (Hussein Mihambo 86’)
FT: KMC 2-3 Namungo (Mwijage 36’, Mohamed 70’ / Ngoy 18’, 24’, 52’)

spot_img

Latest articles

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUFUFUA SKIMU YA MATIPWILI

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema iko tayari kufufua na kuboresha skimu ya Umwagiliaji Matipwili...

Tanzania, AngloGold Ashanti kuimarisha ushirikiano

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa kampuni ya...

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

More like this