Maombi ya Lissu kusikilizwa Juni 2, arudishwa rumande

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga kusilikiza shauri la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu linalohusu maombi ya kuunganishwa katika kesi inayohusu mgawanyo wa mali za chama hicho.

Shauri hilo limetajwa leo Mei 25, 2026, mbele ya Jaji David Ngunyale, ambapo Mahakama imeutaka upande wa wajibu maombi kuwasilisha viapo vyao kinzani ndani ya siku saba.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dk. Rugemeleza Nshala, amesema hatima ya maombi ya Mwenyekiti  huyo itategemea uamuzi unaotarajiwa kutolewa Mei 28, 2026 katika kesi ya msingi iliyorejeshwa Mahakama Kuu kutoka Mahakama ya Rufani.

Ameeleza kuwa, iwapo Mahakama itaamua kesi hiyo inaendelea kuwa na nguvu kisheria, basi maombi ya mwenyekiti yataendelea kusikilizwa, lakini kama kesi ya msingi itafutwa, hata maombi hayo yataathirika.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this