TTB yamkaribisha bingwa wa Masumbwi duniani Terence kwa ziara ya utalii

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amemkaribisha nchini kwa mara ya kwanza bingwa wa masumbwi duniani, Terence Crawford, ambaye katika historia yake hajawahi kupoteza pambano lolote.

Ziara hiyo ya wiki moja nchini imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendeleza utalii wa michezo nchini.

Akizungumza Mei 24,2026, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya mwanamasumbwi huyo, Mafuru amesema Serikali imeamua kutumia watu mashuhuri wenye ushawishi mkubwa duniani kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia sekta ya utalii na michezo.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kukuza utalii wa michezo sambamba na kupata idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini na kuongeza muda wa kukaa kwao.

Mafuru ameeleza kuwa mbali na utalii wa wanyamapori, fukwe, utamaduni na mikutano, Serikali sasa imejikita pia katika kuimarisha utalii wa michezo kama bidhaa nyingine muhimu ya utalii.

Katika ziara hiyo, Crawford anatarajiwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kujionea vivutio vya Tanzania na kuvizungumza katika majukwaa ya kimataifa.

Akizungumzia ujio wake mwana masumbwi huyo ambaye ni raia wa Marekani amesema anafurahi kupata ziara ya wiki moja kujionea utalii na shughuli mbalimbali za michezo.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this