DAWASA yaja na operesheni siku 90 kudhibiti upotevu wa maji

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetenga siku 90 za kutekeleza mpango maalum wa kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma ya majisafi na kuongeza ufanisi wa miundombinu yake.

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa kudhibiti upotevu wa maji, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema Mamlaka imejiwekea siku 90 za kupambana na upotevu wa Maji na hatua za awali zimeanza kwa ukarabati na ubadilishaji wa miundombinu chakavu inayochangia mivujo na upotevu mkubwa wa maji katika maeneo mbalimbali ya kihuduma.

“Kama mnavyofahamu, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) alitoa taarifa kuwa kiwango cha upotevu wa maji katika Mamlaka nyingi nchini kimefikia asilimia 35. Kutokana na hali hiyo, DAWASA tumeanza kuchukua hatua mahsusi kwa kutenga siku 90 za kushughulikia changamoto hii,” amesema Mhandisi Bwire.

Ameeleza kuwa mafanikio ya mpango huo yatategemea ushirikiano wa karibu kati ya DAWASA na wananchi, huku Mamlaka ikiahidi kutoa zawadi kwa watu watakaosaidia kutoa taarifa za mivujo ya maji na maeneo yenye upotevu mkubwa wa huduma hiyo.

“Katika utekelezaji wa mpango huu tutashirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo watumiaji na wasiokuwa watumiaji wa huduma ya maji, pamoja na makundi maalum kama mama lishe, maafisa usafirishaji (Bodaboda), viongozi wa serikali na jamii kwa ujumla,” ameongeza.

DAWASA imebainisha kuwa lengo lake ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kiwango cha upotevu wa maji kinashuka hadi kufikia asilimia 20, kiwango kinachokubalika kimataifa katika sekta ya maji.

Mpango huo unatajwa kuwa sehemu ya mikakati ya muda mrefu ya Mamlaka katika kuboresha usimamizi wa maji, kuongeza mapato, kulinda rasilimali ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika kwa ufanisi zaidi.

spot_img

Latest articles

Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai ghasia za Oktoba 29

Na Mwandishi Wetu RAIS Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa matukio...

Tanesco yatakiwa kubuni teknolojia mpya kuboresha huduma kwa wateja

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, ameielekeza TANESCO kuendelea kufanya tafiti...

Nusu fainali Kombe la shirikisho, Chama atakuwa Arusha, Diarra Mwanza  

Na Winfrida Mtoi MCHEZO wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya...

DAS Temeke azindua ofisi ya Wilaya ya kitanesco ya Mikwambe

📌Aipongeza TANESCO kwa maboresho yanayoendelea ili kusogeza huduma karibu kwa Wananchi. 📌Asema itapunguza adha wananchi...

More like this