Wadau wahimiza ujenzi wa miundombinu ya mchezo wa kuogelea kuendeleza vipaji

Na Winfrida Mtoi

WADAU wa mchezo wa kuogelea nchini, wamefurahishwa na viwango vilivyooneshwa na watoto katika mashindano ya Afrika Mashariki, huku wakiomba serikali kuharakisha ujenzi wa mabwawa yenye viwango vya Olimpiki ili kuviendeleza.

Katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita, yakipewa jina la ‘East Africa Development Swimming Gala’, jumla ya watoto 600 walishiriki, asilimia kubwa wakiwa Watanzania.

Akitoa tathimini ya michuano hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Kuogelea Tanzania (TSA), David Mwansyoge, vipaji ni vingi lakini kikwazo ni miundombinu inayoweza kukusanya watu wengi zaidi.

“Katika mashindano haya tumeona vipaji vingi, kati ya waogeleaji 600, zaidi ya asilimia 50 ni mara ya kwanza wanashindana, hali inayoongeza idadi ya waogeleaji nchini ili kufikia malengo tunahitaji kuwa na miundombinu ya kutosheleza.

“Malengo yetu ni kufikisha waogeleaji zaidi ya 2000, ndio maana tunaendelea kuzungumza na serikali iweze kutujengea sehemu za kuchukua idadi kubwa ya watu na kuwa na eneo la kubeba watazamaji,” ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Prime Sports Agency, Lameck Borega, amesema kukosekana kwa mabwawa ya mita 50 nchini kunawapa changamoto waogeleaji, hasa wanaposhiriki mashindano makubwa nje ya nchi.

“Michezo mingine yote inachezwa nchi kavu lakini kuogelea unachezwa kwenye maji, kwa sababu hiyo lazima kuwe na miundombinu ya maji ambayo ni mabwawa ya kuogelea,”Borega amesema mabwawa ya kuogelea ni gharama kwa mtu binafsi kumiliki.

“Kwa hiyo ningeiomba serikali yetu sikivu, naamini hili linatekelezeka maana serikali yetu inapenda michezo. Nimesikia tayari mabwawa yameanza kijengwa”

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this