Mafuta kupanda bei, serikali yaahidi suluhisho kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli na mafuta mengine ili kuhakikisha bei zake zinaendelea kuwa himilivu, licha ya kuwepo kwa changamoto za kiusalama za kikanda na kimataifa ikiwemo za Mashariki ya Kati zilizosababisha kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Amesema hayo leo Aprili 01, 2026, wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2026/2027 Bungeni, jijini Dodoma.

“Tumeona bei zimeanza kupanda, tutakaa ndani ya Serikali kuweza kuhakikisha tunakabiliana nalo vipi, ili wananchi wananchi wanaendelea kupata mafuta kwa bei wanazoweza kumudu na kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha,” amesema Dkt. Mwigulu.

Katika hatua nyingine, amesema Serikali imeendelea kusimamia mifumo ya kuagiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta, pamoja na kuongeza uwezo wa kupokea na kuhifadhi mafuta katika bandari za Dar es Salaam na Mtwara.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa ghala la kupokea na kuhifadhi mafuta lenye uwezo wa tani 308,110 katika Bandari ya Dar es Salaam, ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 30.

Ameongeza kuwa miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bandari ya Mtwara imeongezeka kutoka tani 29,280 hadi tani 110,221, hatua itakayowezesha kupokea meli yenye shehena ya tani 30,000.

Kwa upande mwingine, amesema Serikali imeendelea kuhakikisha ongezeko la matumizi ya gesi asilia, Katika kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026, mtandao wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia katika viwanda, taasisi na makazi umeongezeka hadi kilomita 243.6, ikilinganishwa na kilomita 184.8 hapo awali.

Amezielekeza Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Nishati kushirikiana kuandaa viwango msawazo (specifications) vitakavyotumika katika mahitaji ya vyombo vya moto vya Serikali, pamoja na kujenga miundombinu ya kutosha ili kuwezesha vyombo hivyo kuanza kutumia gesi asilia iliyoshindiliwa.

spot_img

Latest articles

Latra yawaonya wanaopandisha nauli

Na Mwandishi wetu MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka Wasafirishaji nchini kuwa watulivu...

Petroli, dizeli bei juu kuanzia leo

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei...

Rais Samia: Serikali itachukua hatua yaliyopendekezwa na CAG

Na Mwandishi Wetu RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itachukua hatua kama ilivyoelekezwa na sheria...

TAFF yajipanga kwa Ligi Kuu, Tabora yaanzisha timu

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu...

More like this

Latra yawaonya wanaopandisha nauli

Na Mwandishi wetu MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka Wasafirishaji nchini kuwa watulivu...

Petroli, dizeli bei juu kuanzia leo

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei...

Rais Samia: Serikali itachukua hatua yaliyopendekezwa na CAG

Na Mwandishi Wetu RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itachukua hatua kama ilivyoelekezwa na sheria...