Rais Samia: Serikali itachukua hatua yaliyopendekezwa na CAG

Na Mwandishi Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itachukua hatua kama ilivyoelekezwa na sheria na kama ilivyopendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ili kuondoa mapungufu yaliyobainishwa na CAG kwenye ripoti yake.

Ameeleza hayo leo, Machi 30, 2026, wakati akipokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) katika Ikulu ya Dar es Salaam.

“Nimesikiliza kwa umakini ripoti na taarifa zote zilizowasilishwa nataka nitoe pongezi kwa CAG, Mkurugenzi wa TAKUKURU na PPRA kwa kazi kubwa na nzuri mnazofanya, taarifa zenu zinaonesha mafanikio na mapungufu katika baadhi ya maeneo yanayojitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi kwa kuchukua hatua madhubuti za kurekebisha mapungufu hayo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,”

Amesema kumekuwa na ongezeko la hati safi kwa mwaka 2024/2025, kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, ikilinganishwa na mwaka 2023/2024.

Katika hatua nyingine Rais Samia amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba kuyataja mashirika na taasisi zinazofanya vibaya zaidi katika ripoti ijayo ili waone aibu wafanye vizuri.

“Vilevile nikuelekeze mkurugenzi mkuu PPRA ili tuweze kusimamia vizuri kwenye taasisi zetu, ripoti yako ya mwakani ukitutajia nani anafanya vizuri zaidi na nani wafanya vibaya zaidi itakuwa vizuri na itawatia ari wale wanaofanya vibaya zaidi ili wajitahidi kufanya vizuri,” amesema Rais Samia.

Kuhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),  amesema hali imeimarika, tofauti na ilivyokuwa hapo awali, ingawa baadhi ya dosari zimeendelea kujirudia kila mwaka.

Amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuendelea kuchukua hatua bila upendeleo, kukabili vitendo vya rushwa na ufisadi, na amewaasa viongozi wa serikali na sekta binafsi kuendelea kujiepusha na kupinga rushwa katika maeneo yao ya uwajibikaji.

Aidha amezielekeza wizara tatu ambazo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Fedha na Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kushirikiana kuimarisha matumizi ya mfumo wa NeST ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika taasisi za serikali.

spot_img

Latest articles

TAFF yajipanga kwa Ligi Kuu, Tabora yaanzisha timu

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu...

Bwege afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mkoani Lindi, Selemani Bungara...

Ripoti ya CAG yaibua mazito ujenzi wa uwanja wa AFCON Arusha

Na Mwandishi Wetu RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles...

Deni la Serikali lafikia trilioni 110, mikopo yatajwa

Na Mwandishi Wetu MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema...

More like this

TAFF yajipanga kwa Ligi Kuu, Tabora yaanzisha timu

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu...

Bwege afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mkoani Lindi, Selemani Bungara...

Ripoti ya CAG yaibua mazito ujenzi wa uwanja wa AFCON Arusha

Na Mwandishi Wetu RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles...