NEMC yatoa elimu kwa umma kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Na Tatu Mohamed

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usimamizi sahihi wa taka, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri yanayotarajiwa kufanyika Machi 30 mwaka huu.

Akizungumza katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria NEMC, Hamad Kissiwa, amesema maonesho hayo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia Machi 28 hadi 30, yakilenga kuongeza uelewa wa jamii juu ya thamani ya taka katika uchumi na mazingira.

Amesema maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kubadili mtazamo kuhusu taka, akisisitiza kuwa taka si uchafu bali ni rasilimali muhimu inayoweza kurejelewa na kutumika kama malighafi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.

“Tunawaonesha wananchi kuwa taka zinaweza kuzalisha bidhaa kama nguo, mbolea, chakula cha mifugo na hata kuchangia upatikanaji wa madini kama dhahabu kupitia urejelezaji wa taka za kielektroniki,” amesema Kissiwa.

Ameongeza kuwa kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuangazia tatizo la upotevu wa chakula, akibainisha kuwa taka za chakula ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya gesi chafuzi zinazoathiri mazingira.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, amesema kuwa kati ya asilimia 8 hadi 10 ya hewa chafuzi (greenhouse gases) inachangiwa na taka za chakula.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Mmoja kujionea fursa zilizopo katika sekta ya usimamizi wa taka, ikisisitiza kuwa “taka si uchafu, bali ni mali na fursa ya kiuchumi.”

Katika maonesho hayo, wadau mbalimbali wa mazingira wameshiriki kwa kuonesha ubunifu wao wa kutumia taka kama malighafi ya bidhaa zenye thamani ya kiuchumi, hatua inayochochea ajira na kuongeza kipato kwa wananchi.

Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu kutoka Kampuni ya Chilambo General Trade Company Limited, Maria Michael, amesema kampuni hiyo inajihusisha na ukusanyaji, usafirishaji na utunzaji wa taka hatarishi zikiwemo za kielektroniki, kemikali, mafuta machafu na mabaki ya dawa.

Amesema taka hizo husafirishwa kwenda kwenye viwanda maalum kwa ajili ya kuchakatwa na kutenganishwa kulingana na aina zake ili kurahisisha urejelezaji.

“Katika mchakato huo, vifaa kama chuma, bati na sehemu nyingine za mashine hutenganishwa kwa uangalifu kabla ya kupelekwa kwa wataalamu wa uchakataji. Hata betri za magari na bidhaa za plastiki tunazirejeleza,” amesema.

Aidha, ameeleza kuwa pamoja na shughuli hizo, kampuni hiyo pia hutoa elimu kwa jamii kuhusu usimamizi sahihi wa taka hatarishi ili kulinda afya za wananchi na mazingira.

spot_img

Latest articles

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Naibu Waziri wa Nishati akabidhi vitendea kazi Kwa Tanesco Mkoa wa Shinyanga

📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi 📌Awasihi wananchi kutumia...

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....

Dkt. Mataragio: Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wanaoficha mafuta

Na Tatu Mohamed SERIKALI imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo vya kuficha...

More like this

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Naibu Waziri wa Nishati akabidhi vitendea kazi Kwa Tanesco Mkoa wa Shinyanga

📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi 📌Awasihi wananchi kutumia...

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....