Mwili wa Mwanahabari Mkongwe Makaranga waagwa Dar, kuzikwa Mwanza

Na Mwandishi Wetu

WAANDISHI wa Habari, Wahariri, ndugu na jamaa leo Machi 10, 2026, wamejumuika pamoja katika ibada ya kuaga mwili wa Mhariri Mkongwe, Revocatus Makaranga iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Kimara, Dar es Salaam.

Makaranga ambaye amewahi kufanya kazi na vyombo vya mbalimbali vya habari nchini, alifariki usiku wa kuamkia Machi 5, 2025, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikopelekwa kwa ajili ya matibabu.

Baada ya ibada ya kutoa heshima za mwisho, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho.

Marehemu ni mmoja wa waandishi na wahariri wakongwe nchini waliotoa mchango mkubwa katika tasnia ya habari, akifanya kazi katika vyombo vya habari vya umma wakati wa mfumo wa chama kimoja na baadaye vyama vingi, pia alifanya kazi katika kampuni binafsi za Mwananchi Communications Ltd (MCL), New Habari Ltd.

Makaranga ni mhitimu wa shahada ya uzamili katika uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Wales, Uingereza.

spot_img

Latest articles

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

More like this