UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed

KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Makangarawe wameungana na viongozi wa eneo hilo kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Yombo Dovya, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umetolewa leo Machi 6, 2026 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku hiyo muhimu duniani, ambayo kilele chake hufanyika kila mwaka Machi 8.

Tukio hilo lililenga kuonesha upendo, mshikamano na kujali kundi la watoto wenye mahitaji maalum katika jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Diwani wa Viti Maalum Temeke, Farida Saumu Mkwanywe, ameipongeza UWT Makangarawe kwa kuonesha moyo wa huruma na upendo kwa kuwasaidia watoto hao na kuwapa furaha.

“Nawapongeza sana Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Makangarawe kwa kuonesha moyo wa upendo kwa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Yombo Dovya. Sisi kama viongozi tutaendelea kuwaunga mkono katika juhudi hizi za kijamii,” amesema Mkwanywe.

Kwa upande wake, Katibu wa UWT Makangarawe, Salma Lupinga, amesema kuwa katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu waliamua kutembelea watoto wenye mahitaji maalum ili kushirikiana nao na kuwapa msaada pamoja na walimu wanaowalea.

Amesema UWT Makangarawe imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii kila mwaka, na safari hii waliona ni vyema kusherehekea siku hiyo kwa kuonesha upendo kwa watoto hao pamoja na walimu wao.

Naye Diwani wa Kata ya Makangarawe, Fadhili Mboga, amewapongeza kwa maono yao ya kusaidia jamii na kuwashukuru walimu wanaowalea watoto hao kwa kujitolea kuwasaidia hadi kufikia hatua ya kuendelea na masomo ya sekondari na hata vyuo vya ufundi.

Mboga amesisitiza kuwa wanawake ni nguvu kubwa katika jamii, akieleza kuwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na shughuli za kijamii, wamekuwa mstari wa mbele kutoa huduma na mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii.

Awali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo Dovya alisema kituo hicho kina watoto 100 wenye mahitaji maalum, wakiwemo wavulana 67 na wasichana 33.

Amefafanua kuwa watoto hao wamegawanywa katika hatua tatu za kujifunza, huku wakifundishwa zaidi stadi za maisha zinazowawezesha baadhi yao kuendelea na masomo katika vyuo vya ufundi stadi (VETA).

Kwa upande wake, mwalimu mlezi wa watoto wenye ulemavu, Naghenywa Mshighati, amewashukuru madiwani pamoja na wanawake wa Makangarawe kwa kuwatembelea na kuwapa zawadi watoto hao, akisema kitendo hicho kinaonesha wazi jinsi wanawake walivyo jeshi kubwa katika kuonesha upendo na kujali jamii.

spot_img

Latest articles

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...

Vunjabei, Sara kuisaka heshima ya Tanzania One ulingoni

Na Winfrida Mtoi MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Halima Ramadhani maarufu Vunjabei na Sara Alex...

Mufti Zubeir asisitiza upendo, kupuuza wanaoneza chuki za kidini mtandaoni

Na Mwandishi Wetu MUFTI na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally ametoa...

More like this

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...

Vunjabei, Sara kuisaka heshima ya Tanzania One ulingoni

Na Winfrida Mtoi MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Halima Ramadhani maarufu Vunjabei na Sara Alex...