Vunjabei, Sara kuisaka heshima ya Tanzania One ulingoni

Na Winfrida Mtoi

MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Halima Ramadhani maarufu Vunjabei na Sara Alex wanatarajia kupanda ulingoni Machi 21, 2026 kusaka heshima ya Tanzania One katika pambano litakalopigwa Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Siku hiyo imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kusherehekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, kutakuwa na mapambano mengi yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali kutoka mikoa tofauti.

Akizungumzia maandalizi ya pambano hilo lililopewa jina la Punch kwa Heshima, Halima amesema yeye ni bondia mkubwa, amecheza na mabondia wengi wakubwa hivyo hana hofu na mpinzani wake.

“Huwa sina show mbovu, mabondia wa kike Tanzania wananielewa vizuri, nimepigana nchi kibao nimekutanza na changamoto nyingi nje ya nchi na Watanzania wanaijua kazi yangu. Sara Alex anajua anakwenda kucheza na bondia mkubwa,” ametamba.

Amejinasibu kuwa katika uzoefu wake wa masumbwi amecheza na mabondia wakali wa nje ya nchi na amewahi kutwaa ubingwa wa WBF nchini Ujerumani, ameshinda pambano Afrika Kusini, hivyo hakuna ninachomzuia kupiga mpinzani wake.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this