Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Manyara ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari katika muktadha wa kidijiti.

Mafunzo hayo ambayo ni ya kivitendo zaidi yakiwajumuisha waandishi wabobevu katika tasnia, ni ya siku mbili kuanzia Jumatatu wiki hii.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza wigo wa uelewa katika uandishi wa sasa unaotamalaki katika tekinolojia ya kidijiti.

Yanalenga kuwakumbusha waandishi kwamba katika dunia ya sasa hakuna mwandishi wa habari atakayeweza kutekeleza majukumu yake kama hatajikita kufahamu uandishi wa kidijiti.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni pamoja na mwandishi mkongwe nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Media Brains, Absalom Kibanda, aliyewaeleza waandishi kuwa dunia sasa iko kidijitali zaidi hivyo ni wajibu wa kila mwandishi kutafuta ujuzi na maarifa ya kutumia tekinolojia hiyo ili kuwa na uandishi wenye tija kwa jamii.

Aidha, aliwakumbusha kuwa pamoja na mabadiliko hayo ya tekinolojia, maadili ya uandishi yanabaki vilevile ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria zinazosimamia tasnia ya habari nchini.

Naye Jesse Kwayu, Mkurugenzi wa Media Brains akitoa mafunzo hayo aliwaambia waandishi kuwa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) katika ripoti yake ya Septemba 2025, inaonyesha kuwa watumiaji wa intaneti wamefikia million 49 , huku watumiaji wa simu janja wakiwa ni milioni 27 nchini.

Idadi hiyo ya watu inaeleza kuwa ama ni watumiaji wa vyombo vya habari kwa njia ya kidijitali au wenyewe wanawasiliana kupeana taarifa kwa mfumo wa kidijitali.

Kwayu alisema kwa maana hiyo mfumo wa upataji na upokeaji wa taarifa umebadilika sana kuwa wa kidijiti. Hali hiyo inawalazimu waandishi wa habari kujifunza kwa bidii jinsi ya kutumia tekinolojia hiyo kama wanataka kuendelea na kazi hiyo katika mazingira ya sasa nchini na duniani kote.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...