Mwanasheria Mkuu wa Serikali aongoza zoezi la kutoa huduma za kisheria kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari amewaongoza Mawakili wa Serikali kutoa huduma za ushauri wa Kisheria kwa wananchi wakati wa Kliniki ya Sheria bila malipo iliyozinduliwa tarehe 16 Februari, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Johari amemuhudumia mwananchi aliyekuja kupata huduma ya ushauri wa kisheria ambapo alimsikiliza na kumuhudumia Bi. Sarah Mohamed aliyewasilisha malalamiko yake kuhusiana changamoto ya mirathi inayomkabili.

“Tumeyapokea malalamiko yako na mimi pamoja na timu tutayafanyia kazi kwa haraka ili kuweza kutatua changamoto inayokukabili,” amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika zoezi hilo la kutoa huduma kwa wananchi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab A. Katimba.

Timu ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepiga kambi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutoa huduma mbalimbali za kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 hadi 22 Februari, 2026.

spot_img

Latest articles

VETA Kuongeza Vyuo Kutoka 80 hadi 152 Kufikia 2027

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza mpango...

Kliniki ya Sheria yazinduliwa jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu...

IST Festival yatumika kunadi mitaji nafuu kwa vijana

Na Mwandishi Wetu TAMASHA la IST Festival lililofanyika jana Februari 14, 2026 kwenye viwanja...

Taliss – IST Swimming Championships yawavuta wenye mahitaji maalumu

Na Winfrida Mtoi MASHINDANO ya mchezo wa kuogelea 'Taliss -IST Championship' yameanza leo Februari 14,...

More like this