Dkt. Mwigulu aweka jiwe la Msingi Mradi wa Umeme Mkata

Ni ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme chenye uwezo wa MVA 60

📌Mradi kugharimu takribani bilioni 44.

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 13, 2026 amekagua na kuweka jiwe la msingi la Mradi wa ujenzi kituo cha kupokea na kupoza umeme cha MVA 60 Mkatata Tanga na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovolti 33.

Akiweka jiwe la msingi mradi huo, Dkt. Mwigulu amesema kutekelezwa kwa mradi huo ni jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika.

“Nitoe rai kwa Wizara ya Nishati kuhakikisha kasi ya ukamilishwaji wa mradi huo na unakamilika kwa wakati,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine ameiagiza Wizara ya Nishati kuwasiliana na Wizara ya Fedha ili kukamilisha malipo ya fidia kwa Wananchi takribani shilingi bilioni moja.

Ujennzi wa mradi huo ni shilingi bilioni 44 na unahusisha ujenzi wa vituo viwili vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme vyenye uwezo wa MVA 60 huku kila kimoja kikiwa na MVA 30, pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 33 kutoka kituo cha Mkata hadi kwa Msisi.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemshukuru Rais kwa kuwezisha upatikanaji wa fedha zitakazo tumika katika utekelezaji wa mradi huo.

“Utekelezaji wa mradi huu unakwenda kuondoa changamoto za umeme katika Wilaya za Handeni na Kilindi ambazo zinapata umeme kutokea Tanga mjiani ambapo ni umbali mrefu,” amesema Ndejembi.

Amefafanua kuwa kupitia miundombinu hiyo mipya, umeme utasafirishwa kutoka Mkata kwenda Msisi kwa umbali wa kilomita 45, hatua itakayoongeza uwezo wa usambazaji na kuimarisha huduma katika maeneo hayo.

Kuimalika kwa huduma ya umeme Wilaya za Handeni na Kilindi kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii.

spot_img

Latest articles

CRDB na Costech watenga Sh. Bilioni 4.6 kuwezesha mitaji kwa vijana wabunifu

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia TUME ya Sayansi na...

Wanahabari watakiwa kuweka usawa katika uandishi wa mabadiliko ya tabianchi

Na Tatu Mohamed MWAKILISHI wa kimataifa kutoka ActionAid International, Teresa Anderson, amesema ipo haja...

Ithibati yatajwa kuimarisha uaminifu wa Sekta ya Habari na Uchumi wa Vyombo vya Utangazaji

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema utekelezaji wa mfumo...

Tunasogeza huduma za kisheria karibu zaidi na wananchi- Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ametoa wito kwa wananchi...

More like this