Dkt. Mwigulu ataka ushirikiano wa kikanda kwenye mapambano dhidi ya saratani

▪Asisitiza Tanzania itaendelea kuwa kituo bora cha ushirikiano wa kikanda na Afrika

▪Asema shilingi bilioni 18.5 zimetengwa kwa ajili ya uanzishaji wa huduma za PET-CT Scan na mashine ya Cyclotron

▪Asema Tanzania inalenga kupunguza vifo vitokanavyo na saratani kwa angalau asilimia 30 ifikapo mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Afrika haiwezi kushinda vita dhidi ya saratani ikiwa kila nchi itafanya kazi peke yake.

Amesema kuwa ili kufikia malengo ya mapambano dhidi ya saratani, kunahitajika kuwepo kwa ushirikiano wa kikanda na wa bara zima katika utafiti, mafunzo, kubadilishana wataalamu na kubadilishana rasilimali, teknolojia pamoja na uzoefu.

Ametoa wito huo leo Alhamisi (Februari 12, 2026) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi ya Saratani Ocean Road, yanayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na nchi zote za Afrika na kupitia Taasisi ya Saratani Ocean Road tutaendelea kuwa kituo cha ushirikiano wa kikanda na bara zima katika mapambano dhidi ya saratani” amesema.

Dkt. Mwigulu amesema kuwa kupitia simulizi za machapisho ya kitafiti na sayansi ambazo wataalamu wa Taasisi ya Saratani Ocean Road na Tanzania kwa ujumla wameyafanya, yamekuwa na mchango mkubwa ndani na nje ya nchi kisera na kiutendaji katika mapambano dhidi ya saratani.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu ameiagiza Wizara ya Afya kuandaa mkakati madhubuti wa kupunguza idadi ya wagonjwa wapya wa saratani ili kupunguza athari kwa rasilimaliwatu, uchumi na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

“Kutokana na tahadhari ya wataalamu wa afya kutoka Shirika la Afya Duniani kuhusu ugonjwa wa saratani kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 ifikapo mwaka 2030, Wizara ya Afya mnapaswa kuandaa mikakati ya kupunguza idadi ya wagonjwa wapya.” amesema.

Pia, Dkt. Mwigulu amesema kuwa Serikali kwa kutambua athari za ugonjwa wa saratani kwa ustawi wa nguvukazi ya Watanzania, imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka mifumo mizuri ya kisera, kutekeleza mipango na mikakati muhimu dhidi ya ugonjwa huo.

“Serikali kwa kutambua athari za ugonjwa wa saratani kwa ustawi wa nguvukazi ya Watanzania imeimarisha wigo wa upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa awali wa saratani za aina mbalimbali ikiwemo; saratani ya mlango wa kizazi, matiti, tezi dume na utumbo hadi katika ngazi ya msingi”.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua kuwa afya si huduma pekee, bali afya ni haki, heshima, na ni ndoto za familia kwani mapambano dhidi ya saratani ni agenda ya Taifa si mzigo kwa mtu mmoja.”

“Maendeleo ya kweli hayapimwi kwa maneno bali kupata huduma kwa karibu, haraka na usawa, katika eneo la saratani, tumaini hili linaonekana kwenye kasi ya maboresho ya mifumo na utoaji huduma, uongozi wa Rais Dkt. Samia umeifanya afya kuwa ni ajenda ya Taifa na tutaendelea kuleta faraja kwa Watanzania kwenye sekta ya afya” amesema.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt. Diwani Msemo amesema wanaposherehekea miaka 30 ya Taasisi hiyo wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kufanya mageuzi makubwa yaliyofanyika.

“Kuna mengi yamefanyika lakini ukweli haupingiki uwekezaji uliofanyika ndani ya miaka mitano iliyopita ni mkubwa.

“Kwetu sisi sio sherehe tu bali tunajivunia dhamira yetu ya kuendeleza kuokoa maisha ya Watanzania dhidi ya ugonjwa huu wa saratani” amesema Dkt. Msemo

spot_img

Latest articles

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

More like this

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...