Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna mechi rahisi ya Ligi Kuu, lakini wamejipanga kuhakikisha wanachukua pointi katika mchezo wao wa kesho dhidi ya KMC utakaopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenye jijini Dar es Salaam.

Barker amesema anawaheshimu wapinzani, lakini  wamejiandaa na wachezaji wake wanaonekana kujitoa kwa kila mechi na kiwango cha timu kinaendelea kuimarika kila mchezo pamoja na wachezaji wengi wapya.

Amesema baada ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika walirejea kufanya maandalizi mchezo wa kesho ambao ni muhimu kwao kupata ushindi ili kuimarisha nafasi yao katika msimamo wa Ligi Kuu.

“Maandalizi yanakwenda vizuri hadi sasa, tunahitaji kucheza mechi hii vizuri ili kupata ushindi unaotakiwa kama malengo yetu tulijiwekea,” amesema kocha huyo.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa KMC, Mohamed Abdallah ‘Bares’ amesema wanajua wanakwenda kucheza mchezo mkubwa, pia bado wana presha kutokana na kuwa katika hali ya chini kwa sababu ya kushindwa kupata matokeo mazuri,

 “Kesho tunaingia kwa kutuliza presha kwa mashabiki paamoja na wachezaji wetu, naamini presha itaondoka kutokana na matokeo tutakayopata katika mchezo huo. Kikubwa ni wachezaji kuwa makini,” amesema Bares.

Katika msimamo wa ligi hiyo Simba ipo nafasi ya saba na pointi 16, ikicheza mechi saba, wakati KMC  inaburuza mkia na  pointi nane ilizokusanya katika michezo 14, ikishinda mechi mbili pekee hadi sasa.

spot_img

Latest articles

Rais Mwinyi akagua Mji wa AFCON Fumba

Na Mwandishi WetuRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Sowah apigwa faini nzito  kwa utovu wa nidhamu, ashushwa U-20

Na Winfrida Mtoi UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka wazi hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa...

Waziri Mavunde aelekeza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji Busulwangili-Kahama – Kahama

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza kusimamishwa mara moja kwa...

DC Mkude akabidhi vyombo vya usafiri Tanesco Mkoa wa Arusha kuimarisha utoaji huduma

📌 Ni katika muendelezo wa mkakati wa TANESCO wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi. 📌...

More like this