Wawili wajeruhiwa ajali ya moto Dar

Na Mwandishi Wetu

WATU wawili wamejeruhiwa kutokana na ajali ya moto iliyotokea leo Januari 16,2025 katika jengo la NSSF lililopo katika mtaa wa Azikiwe na Samora, Posta,Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi la uokoaji Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala, Frank Mwalongo amethibitisha kujeruhiwa kwa watu  hao wawili ambao wamewahishwa hospitali ya Mnazi Mmoja kwa huduma ya kwanza.

“Majira ya saa sita na robo mchana tulipokea wito wa dharura kuhusu ajali ya moto katika jengo la NSSF, na walifanikiwa kufika eneo la tukio kwa wakati na kuweza kupambana na moto huo na kuudhibiti,” amesema.

Ameeleza kuwa ajali hiyo haijaleta madhara makubwa kwa jengo ambapo ghrofa  ya kwanza ya jingo ndiyo imeathirika kidogo, lakini mali zimeokolewa na watu wote walikuwemo ndani wako salama.

Mwalongo amesema bado chanzo cha moto huo hakijajulikana, uchunguzi  unaendelea na ukikamilika taarifa rasmi itatolewa.

spot_img

Latest articles

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

More like this