Na Mwandishi Wetu
YANGA imetwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi ikiifunga Azam FC kwa mikwaju ya penalti 5-4 katika mchezo wa fainali uliopigwa Januari 13, 2026 kwenye dimba la Gombani, Pemba.
Mchezo huo uliishia kwa sare tasa ndani ya dakika 90 za kawaida, hali iliyomlazimu mwamuzi kuongeza muda wa nyingeza dakika 30 ili kumpata mshindi, lakini hakuna timu iliyofanikiwa kufunga.
Katika dakika ya 115 ya mchezo, Yanga ilipata penalti lakini kipa wa Azam Aishi Manula aliokoa mkwaju huo uliopigwa na Pacôme Zouzoua, huku Azam ikiwa pungufu.
Mchezo huo ulikuwa ni mgumu kwa pande zote, licha ya Azam kucheza pungufu tangu dakika ya 74 baada ya mchezaji wao Cheikna Diakite kuoneshwa kadi nyekundu.
Aidha Max Nzengeli wa Yanga amekiwa mchezaji bora wa mashindano (MVP), Manula kipa bora na Jephte Kitambala wa Azam akiibuka mfungaji bora.


