Chongolo akutana na wawekezaji  kutoka China

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Kilimo, Daniel Chongolo, amekutana na wawekezaji kutoka nchini China  na kujadili uwekezaji katika Sekta ya Kilimo hususan kuongeza uzalishaji wa mazao, thamani na kuleta teknolojia za kisasa zitakazoleta tija kwa wakulima.

Mkutano huo umefanyika Januari 5, 2026, jijini Dar es Salaam ambapo wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza katika mazao ya kimkakati, likiwemo zao la korosho, kuanzia uzalishaji hadi uongezaji wa thamani wa zao hilo.  

Akieleza zaidi kuhusu majadiliano yao, Waziri Chongolo amesema kuwa wawekezaji pia wamehamasishwa kuwekeza katika uzalishaji wa mafuta ya korosho, methanol na bidhaa nyingine.  Eneo lingine ni zao la Soya kwa ajili ya chakula cha binadamu na mifugo, hatua itakayosaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vya ndani.

Majadiliano hayo pia yalilenga kilimo cha vitunguu na uwekezaji katika mashine zinazorahisisha utengenezaji wa matuta kwa wakulima wa mpunga ili kupunguza muda na gharama za kazi shambani. 

Kwa niaba ya timu ya wawekezaji, Bw. Li Qingyu amesema uwekezaji wao utalenga kuongeza uzalishaji, kuhamisha teknolojia ya kisasa kwa wakulima, kuongeza ujuzi na kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha uongezaji wa thamani wa mazao ya kilimo. 

Waziri Chongolo amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje waliolenga kuongeza thamani ya mazao na kuimarisha teknolojia ya kisasa katika kilimo.

spot_img

Latest articles

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

2025 mwaka wa mageuzi na matokeo katika mashirika ya umma

Na Mwandishi Wetu MWAKA 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Ofisi ya Msajili wa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...

Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu...

More like this