Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Arthur Nanauka amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, toleo la 2024, kwa kuzingatia maeneo 13 ya kipaumbele ikiwemo elimu ya ufundi stadi, uchumi wa kidijitali, ubunifu, uongozi, afya, usawa wa kijinsia na ujumuishwaji wa vijana wenye ulemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema vijana ni rasilimali kubwa ya Taifa, ambapo takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinazoonesha kuwa vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 ni zaidi ya milioni 20.6, sawa na zaidi ya asilimia 55 ya nguvu kazi ya nchi.

“Serikali imejipanga kikamilifu kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii kwa kuwafikia walipo, kuwasikiliza na kuwashirikisha katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya Taifa.

“Mwelekeo wa Serikali ni kuifuata dira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza ajenda ya ajira, ujuzi, uzalishaji na matumizi ya teknolojia, ili vijana wanufaike na fursa za uchumi wa sasa na wa baadaye,” amesema Nanauka.

Amebainisha kuwa hatua hizo zinaendana na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025–2030, inayolenga kuzalisha ajira zisizopungua milioni nane ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.

Aidha ametaja changamoto kuu zinazowakabili vijana kuwa ni ukosefu wa ajira zenye staha, upungufu wa ujuzi unaohitajika sokoni na ukosefu wa mitaji kwa vijana wajasiriamali na kampuni changa, akisema Serikali imejipanga kukabiliana nazo kupitia sera na mikakati mbalimbali.

Akizungumzia ajira, amesema Serikali inaandaa mikakati ya kuongeza fursa za kazi ndani na nje ya nchi, kuimarisha huduma za ajira na kulinda haki za vijana wanaoajiriwa nje, sambamba na kuendeleza programu za mafunzo kazini na uzoefu wa kazi kupitia mifuko ya maendeleo ya ujuzi.

Ameongeza kuwa Serikali inawekeza katika sekta zenye ajira nyingi ikiwemo kilimo-biashara, madini, uvuvi na viwanda, pamoja na kuimarisha uwekezaji kupitia kongani na maeneo maalumu ya kiuchumi ili kuongeza ajira na ujuzi kwa vijana.

Katika kuwezesha mitaji, Waziri Nanauka amesema Serikali imeanza kuimarisha mifumo ya dhamana ya mikopo ili kuwasaidia vijana wengi wanaokosa dhamana kupata mikopo, pamoja na kusimamia kutengwa kwa asilimia 30 ya ununuzi wa umma kwa makundi maalumu ikiwemo vijana.

“Tutaanzisha pia jukwaa la kidijitali la huduma jumuishi kwa vijana (Youth Digital One Stop Platform) litakalowaunganisha vijana na taarifa za ajira, mafunzo, mikopo na masoko, kama sehemu ya kutumia teknolojia kurahisisha upatikanaji wa huduma,” ameeleza.

Amesema pia Serikali itaendelea kuimarisha majukwaa ya ushiriki wa vijana kama VIJANA Platform, pamoja na kufufua vituo vya maendeleo ya vijana vya Sasanda, Ilonga na Marangu ili kutoa ujuzi wa vitendo, nidhamu na stadi za ujasiriamali.

Amewataka vijana wa Tanzania kuwa wazalendo, wachapakazi na wenye nidhamu, wakilinda amani na mshikamano wa Taifa, huku akisisitiza kauli mbiu ya “Vijana Tuyajenge, Tanzania ni Yetu,” akiahidi kuwa ofisi yake iko wazi kwa ajili ya kusikiliza na kuhudumia vijana wote.

spot_img

Latest articles

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

Serikali yaahidi kuimarisha uwezeshaji wa Makundi Maalum kupitia ajenda ya Maendeleo Jumuishi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt....

Mavazi ya kitamaduni kivutio kingine AFCON 2025

Na Winfrida Mtoi SHAMRASHAMRA kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2025), zimezidi kupamba moto, hasa baada...

More like this

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

Serikali yaahidi kuimarisha uwezeshaji wa Makundi Maalum kupitia ajenda ya Maendeleo Jumuishi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt....