Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda na biashara inaendelea kuwa chachu ya ajira na fursa za kiuchumi kwa vijana, hususan kupitia upanuzi wa masoko ya kimataifa na uimarishaji wa uzalishaji wa ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 18, 2025 jijini Dar es Salaam, Waziri Kapinga amesema uwepo wa masoko ya kimataifa unatoa fursa kubwa kwa vijana kuanzisha na kuendesha biashara za kuuza bidhaa za Tanzania nje ya nchi.

Ameongeza kuwa Serikali iko katika hatua za mwisho za kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Mauzo ya Nje, unaolenga kuwashirikisha vijana kikamilifu katika utekelezaji wake.

Kwa mujibu wa Waziri Kapinga, takwimu za mwaka 2024 zinaonesha sekta ya viwanda kuchangia asilimia 7.3 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2023, huku kasi ya ukuaji wa sekta hiyo ikiongezeka kutoka asilimia 4.3 mwaka 2023 hadi asilimia 4.8 mwaka 2024.

“Sekta ya biashara imeongeza mchango wake kutoka asilimia 8.4 mwaka 2023 hadi asilimia 8.6 mwaka 2024, huku ukuaji wake ukifikia asilimia 4.8.“Ongezeko hili limetokana na maboresho ya mazingira ya biashara, upanuzi wa viwanda pamoja na juhudi za Serikali kufungua masoko mapya ya kikanda na kimataifa,” amesema Waziri Kapinga.

Amebainisha kuwa thamani ya bidhaa zilizozalishwa viwandani ilifikia shilingi bilioni 26,438.5 mwaka 2023 kutoka shilingi bilioni 25,034.5 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 5.6.

Akizungumzia masoko ya nje, Waziri Kapinga amesema mauzo ya bidhaa za Tanzania barani Afrika yalifikia Dola za Marekani bilioni 3.94 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 40, yakihusisha bidhaa kama kahawa, tumbaku, vioo, nafaka, viungo na nyuzi za mkonge.

Ameongeza kuwa masoko mapya yamefunguliwa kupitia Mkataba wa Biashara Huria wa Afrika (AfCFTA), yakiwemo Nigeria, Morocco, Senegal, Ethiopia, Ghana, Algeria, Djibouti na Guinea.

“Kwa soko la Umoja wa Ulaya, mauzo yameongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 633.5 mwaka 2023 hadi milioni 686.3 mwaka 2024, huku soko la Asia likirekodi mauzo ya Dola za Marekani bilioni 2.84 mwaka 2024 yakijumuisha bidhaa kama korosho, mazao ya kunde, parachichi, pamba, karanga na nyama ya mbuzi,” amefafanua.

Katika hatua nyingine, Waziri Kapinga ametoa wito kwa wazalishaji na wawekezaji kuendelea kuimarisha uzalishaji wa bidhaa bora viwandani ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.

Amesema uzalishaji wa ndani ni nguzo muhimu katika kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje.

Amebainisha kuwa baadhi ya viwanda vya saruji, marumaru na mabati tayari vimeongeza uzalishaji na kusambaza bidhaa kwa wingi sokoni, hatua inayochangia upatikanaji wa ajira na ukuaji wa uchumi.

Aidha, alisema Serikali inaendelea kuweka sera na mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazokabili sekta hiyo ikiwemo uhaba wa nishati, gharama za malighafi na changamoto za usambazaji wa bidhaa.

Waziri Kapinga pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wawekezaji, wajasiriamali wadogo na mamlaka za udhibiti ili kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinakidhi viwango vya ubora na usalama.

Ameeleza kuwa, ushirikiano huo utasaidia kuongeza thamani ya bidhaa za ndani, kukuza biashara na kutoa fursa zaidi za ajira kwa vijana.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uzalishaji ili sekta ya viwanda na biashara iendelee kuwa mhimili mkuu wa maendeleo ya uchumi wa Taifa,” amesema.

spot_img

Latest articles

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kwa AFCON 2025

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na...

CRDB yashirikiana na Kids’ Holiday Festival kukuza elimu ya fedha kwa watoto

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kids’ Holiday Festival...

Katibu Mkuu Kiongozi awataka maofisa habari serikalini kujiimarisha kiutendaji kukabiliana na teknolojia

Na Winfrida Mtoi KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka amewataka Maofisa Habari wa Serikali...

More like this

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kwa AFCON 2025

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na...

CRDB yashirikiana na Kids’ Holiday Festival kukuza elimu ya fedha kwa watoto

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Kids’ Holiday Festival...