Balozi Bandora kuzikwa kesho makaburi ya Kinondoni

Mwanadiplomasia nguli wa Tanzania, aliyewahi  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Eswatini na Namibia, Timothy Bandora (72),  anatarajia kuzikwa kesho Desemba 16, 2025, katika Makaburi ya Kinondoni.

 Balozi  Bandora alifariki dunia  wiki iliyopita   akiwa jijini Nairobi, nchini Kenya, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Aliitumikia Serikali kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu, alitekeleza majukumu mbalimbali ya kitaifa na kimataifa katika utumishi wa umma pamoja na ndani ya Umoja wa Mataifa (UN), akihudumu katika nyadhifa tofauti kwa uadilifu na weledi mkubwa.

Kwa mujibu wa ratiba ya msiba iliyotolewa na familia, ibada ya mazishi itafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Msasani, jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa majukumu aliyofanya wakati wa uhai wake ni kuongoza kurugenzi ya ushirikiano wa kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ofisi ya Lagos, ambayo pia inahudumia nchi za Benin, Togo, Cote d’Ivoire, Ghana, Guinea, Senegal, Burkina Faso, Mali, Sierra Leone, Liberia, Guinea-Bissau na Mauritania.

spot_img

Latest articles

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

More like this

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...