Bokya amtahadharisha mapema Tyson wa Bongo

Na Winfrida Mtoi

Bondia Ismail Khalid maarufu Boyka ametamba kutoa kipigo kikali kwa mpinza wake Hassan Ndonga ‘Tyson Wa Bongo’  hadi  aombe maji ulingoni.

Bokya ameyasema hayo wakati wa mazoezi kuelekea pambano lao la siku ya Boxing On Boxing Day, Desemba 26,2025 House Masaki Jijini Dar es Salaam, usiku ambao Hassan Mwakinyo atazichapa Stanley Eribo kutoka Nigeria.

Ametamba kuwa fedha itampoza na walimtuma hawajamuambia ukweli ni kipigo gani atakakutana nacho, hivyo kumtahadharidha ikiwezekana asipande ulingoni siku hiyo.

“Ninachomuambia Hassan Ndonga, yaani nitakupiga nitakupakua, sina fomula napiga kushoto napiga kulia. Katika mabondia niliocheza nao hakuna hata mmoja Hassan Ndonga amecheza naye,” ametamba Bokya.

Kwa upande mashabiki wa bondia huyo walikuwa wakimsapoti mazoezini hapo, amesema maandalizi anayofanya bondia wao, mpinzani hawezi kufika hata raundi nne za mchezo.

Mabondia wengine watakaopanda ulingini siku hiyo ni Hamadi Furahisha akizichapa dhidi ya Mmalawi Hanock Phiri, Ally Ngwando na Mussa Makuka, Issa Simba wa Kahama dhidi ya Wilson Phiri Wa Malawi, huku wanawake ni Hidaya Zahoro dhidi ya Leila Macho, Debora Mwenda kuzichapa na Mmalawi Mariam Dick.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this