Mnyama Simba afia kwa Mkapa, Yanga, Azam kicheko

Na Winfrida Mtoi

LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea leo Novemba 7, 2025 kwa michezo miwili kupigwa ambapo Yanga na Azam zimefanikiwa kuondoka na alama tatu kila mmoja, huku Mnyama Simba akiambulia kichapo.

Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Coastal Union kwenye dimba la Jamhuri Dodoma, wakati Azam imeipiga Simba mabao 2-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Prince Dube dakika ya 88, huku mabao ya Azama yakifungwa na Jephte Kitambala dakika 81 na Idd Seleman ‘Nado’ dakika ya 89.

Matokeo ya Simba yamewafanya mashabiki wake waondoke uwanjani kwa hasira huku wakiwatupia lawama viongozi wa klabu hiyo.

Kocha wa Simba Selemani Matola ametaja kile kilichowaangusha kuwa ni kupoteza umakini kwa wachezaji wake dakika za jioni.

Kwa upande wake kocha wa Azam FC, Florent Ibenge amesema mchezo ulikuwa mgumu lakini mabadiliko aliyofanya kipindi cha pili yamempa matokeo mazuri.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

More like this