Serikali yawaita wadau kujitokeza kusapoti ushiriki wa wanawake michezoni

Na Winfrida Mtoi

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ amewaomba wadau na wadhamini kujitokeza kusapoti ushiriki wa wanawake katika michezo ili kuweka uwiano sawa na wanaume.

Amesema ushiriki wa wanawake katika riadha kwa Tanzania bado ni mdogo ukilinganisha na wanaume, hali inayochangiwa na majukumu mengi kwa mwanamke.

Amezungumza hayo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya riadha kwa wanawake maafuru Ladies First, yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

MwanaFA amesema kuna ni muhimu kuungana pamoja kuhakikisha dhana potofu inayozuia wanawake kushiriki michezo inaondolewa, huku akisisitiza kufanyika kwa mashindano mengi yanayoshirikisha wanawake.

Naibu waziri huyo ameeleza kuwa jamii inatakiwa kutambua kuwa kwa michezo ni ajira, inakuza uchumi na Serikali ina matumaini makubwa ya vipaji vipya vinavyoibuliwa kupitia mashindano hayo.

Akizungumzia Ladies First ameleza kuwa, mashindano hayo yamekuwa katika kuandaa wanariadha watakaoiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ikiwamo ya Kimataifa.

“Niwapongeze sana JICA, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kwa kuendesha mashindano haya kwa mafanikio makubwa. Yamekuwa yakifanyika kwa msimu wa saba sasa,” amesema.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msitha ameeleza kuwa heshima kubwa anampa muasisi wa mashindano hayo, mwanariadha mkongwe Kanali Mstaafu Juma Ikangaa kutokana na kuona umuhimu wa kuwapa nafasi wanawake kushiriki riadha.

spot_img

Latest articles

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...

More like this