Ridhiwani:Niko tayari kuhojiwa kuhusu tuhuma za Lake Oil

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesema yuko tayari kuitwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kujibu tuhuma zinazomhusisha na umiliki wa vituo vya mafuta vya Lake Oil.

Amesema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo Novemba 26, 2025, akibainisha kuwa ni muhimu taarifa za watumishi wa umma kuwa wazi.

Amesisitiza kuwa pale panapojitokeza sintofahamu, viongozi wanapaswa kuhojiwa na taarifa kuwekwa hadharani ili wananchi wapate ukweli.

“Malalamiko juu ya viongozi yamekuwa mengi sana; haijulikani lipi ni kweli na lipi si kweli,” amesema.

Akitoa mfano, Ridhiwani amesema maandamano yaliyotokea hivi karibuni yalihusisha malalamiko kuhusu maadili ya viongozi, ambapo ilidaiwa kuwa vituo vya mafuta vinavyojulikana kama Lake Oil vinamilikiwa naye.

“Kuna mtu mmoja anaitwa Ali Edha; ana vituo vya mafuta vinavyoitwa Lake Oil, lakini vimechomwa kwa madai kuwa ni vya Ridhiwani,” amesema.

Ridhiwani aliitaka tume hiyo kumuita bila hofu ili kumhoji, huku akipendekeza uchunguzi ufanyike kwanza na baada ya kukamilika waandaliwe waandishi wa habari. Pia alishauri tume iombe ushahidi wa ziada kutoka kwa umma ili kuweka ukweli hadharani.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this