Rais Samia atangaza Baraza Jipya la Mawaziri, nane watemwa

Tatu Mohamed na Winfrida Mtoi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza Baraza jipya la Mawaziri leo Novemba 17, 2025, ambapo amefanya mabadiliko makubwa ikiwemo kuwaondoa mawaziri nane waliokuwa kwenye baraza lililopita.

Walioachwa katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, pamoja na mawaziri: Hussein Bashe (Kilimo), Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani), Jenista Mhagama (Afya), Dk. Seleman Jafo (Viwanda na Biashara), Dk. Pindi Chana (Maliasili na Utalii), Dk. Damas Ndumbaro (Katiba na Sheria) na Stergomena Tax (Ulinzi).

Baraza hilo jipya lina mawaziri 27 na manaibu mawaziri 29 katika wizara 27.

Katika Baraza hilo jipya aliyechukua nafasi ya Dk. Biteko Wizara ya Nishati ni Deogratius Ndejembi, Mrithi wa Bashe ni Daniel Chongolo, Wizara ya Mambo ya Ndani huku George Simbachawene akichukua nafasi ya Bashungwa.

Rais Samia amemteua Raymond Nyansao kuwa Waziri wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akichukua nafasi ya Stergomena Tax huku Wizara ya Maliasili na Utalii aliyokuwepo Pindi Chana akimteua Dkt. Ashatu Kijaji.

Wizara ya Viwanda na Biashara iliyokuwa chini ya Dkt. Jafo amemteua Judith Kapinga huku nafasi ya Ndumaro Wizara ya Katiba na Sheria ikichukuliwa na Juma Homera.

Mawaziri wapya ni Balozi Hamis Mussa Omary ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha akichukua nafasi ya Dk. Mwigulu Nchemba ambaye wiki iliyopita aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joel Nanauka kuwa Waziri wa Vijana, Balozi Dk. Bashiru Ally (Waziri wa Mifugo na Uvuvi) na Daniel Chongolo (Waziri wa Kilimo).

Mawaziri waliobakishwa kwenye Wizara zao ni Mahmood Thabit Kombo (Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano na Afrika Mashariki), Anthony Mavunde (Wizara ya Nishati), Prof. Palamaganda Kabudi (Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo), Adolf Mkenda (Wizara ya Elimu), Dorothy Gwajima (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum), Jumaa Aweso (Wizara ya Maji), Kitila Mkumbo (Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji), Prof. Makame Mbarawa (Wizara ya Uchukuzi) na Abdallah Ulega (Wizara ya Ujenzi).

Waliorejeshwa na kuhamishwa Wizara, ni Ridhiwani Kikwete, Mhandisi Hamad Masauni, Deogratius Ndejembi, Judith Kapinga, George Simbachawene na Dkt. Ashantu Kijaji.Kwa upande wa Manaibu Waziri walioteuliwa ni Zainabu Katimba (Wizara ya Katiba na Sheria), Salome Makamba (Wizara ya Nishati), Dkt. Steven Kiruswa (Wizara ya Madini), Ngwasi Kamani (Wizara ya Mifugo na Uvuvi), Hamis Mwinjuma na Paul Makonda (Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Hamad Hassan Chande (Wizara ya Maliasili na Utalii), Kasper Muya ( Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Wanu Hafidhi Ameir (Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia) na Dkt. Florance Samizi (Wizara ya Afya).Wengine ni Marry Mahundi (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum), Sweetbert Mkama(Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Patrobas Katambi (Wizara ya Viwanda na Biashara), David Mwakiposa (Wizara ya Uchukuzi), Godfrey Msonge (Wizara ya Ujenzi), Kundo Mathew (Wizara ya Maji), David Silinde (Wizara ya Kilimo), Denis Londo (Wizara ya Mambo ya Ndani), Dkt. Ngwaru Magembe na James Millya (Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano na Afrika Mashariki).Pia Laurent Luswetula na Mshamu Munde (Wizara ya Fedha), Reuben Nhamanilo na Dkt. Jaffar Rajab Seif (Tamisemi), Rahma Kisuo (Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano), Ummy Nderiananga (Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. festo Dugange (Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira), Pius Chaya (Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji) pamoja na Regina Kwarai (Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

spot_img

Latest articles

MC Pilipili afariki dunia

Na Mwandishi Wetu Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' amefariki dunia leo,...

Watahiniwa 595,816 kuanza Mtihani wa Kidato cha Nne kesho

Na Tatu Mohamed JUMLA ya watahiniwa 595,816 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025...

Tume kuundwa kuchunguza vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu

Na Mwandishi Wetu  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza...

More like this

MC Pilipili afariki dunia

Na Mwandishi Wetu Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' amefariki dunia leo,...

Watahiniwa 595,816 kuanza Mtihani wa Kidato cha Nne kesho

Na Tatu Mohamed JUMLA ya watahiniwa 595,816 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025...