Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na viongozi wengine wa chama hicho wameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi jioni ya leo jumatatu Novemba 10, 2025.
Heche ameachiwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho akiwemo Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa, Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani Boniface Jacob na Mjumhe wa Kamati Kuu Godbless Lema.
Kwa mujibu wa wakili Hekima Mwasipu amesema Heche ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi toka Oktoba 22, 2025 alipokamatwa katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Amesema viongozi wote hao wameachiwa katika kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam


