Lissu anyimwa dhamana, kesi yaahirishwa hadi Nov 3

Na Mwandishi Wetu

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu imeahirishwa leo Oktoba 24 hadi Novemba 3, 2025,.

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mfululizo tangu Oktoba 6, 2025 imeahirishwa baada ya upande wa Jamhuri kuomba kuahirisha shauri hilo ili kupisha uchaguzi mkuu ambao upo kwa mujibu wa Katiba.

Awali, mshitakiwa Tundu Lissu, aliiomba Mahakama kutoahiriahwa kwa kesi hiyo na kama Mahakama itakubali ombi la upande wa Jamhuri basi yeye apewe dhamana kwa mujibu wa kifungu  302(3) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), hadi tarehe iliyopangwa kwenye ratiba ya usikilizaji wa kesi hiyo.

Lissu aliwasilisha ombi hilo leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025, mara baada ya Jamhuri kuiomba Mahakama kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo hadi Novemba 3, 2025, kwa maelezo kuwa mashahidi waliopangwa kutoa ushahidi wao leo wanahusiana na vielelezo vilivyokataliwa wiki hii.

Baada ya kusikiliza ombi la pande zote mbili, Jopo la majaji likiongozwa na Dustan Nduguru limekuja na maamuzi ya kuahirisha kesi hiyo huku wakisema ombi la mshitakiwa kuomba dhamana haliwezekani kwani kesi inayomkabili (Uhaini), haina dhamana.

spot_img

Latest articles

Mnyama Simba afia kwa Mkapa, Yanga, Azam kicheko

Na Winfrida Mtoi LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea leo Novemba 7, 2025 kwa michezo miwili...

Waziri Aweso aweka kambi Dar kupambana na changamoto upungufu wa maji

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) amefanya ziara ya kikazi katika...

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

More like this