Msanii aiombea michango Tembo Warriors, yakusanya sh. 270,000 pekee

Na Winfrida Mtoi

Msanii wa Bongo Flava, Frank Humbuchi maarufu Foby amewataka watanzania na wasanii wenzake kuichangia timu ya Taifa ya Soka kwa watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ ili kuiwezesha kushiriki Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)yatakayoanza Septemba 8 -14, 2025 nchini Burundi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 1, 2025, jijini Dar es Salaam, Foby  amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anaiwezesha timu hiyo kushiriki mashindano hayo kama wanavyofanya katika timu nyingine.

“Niwaombe wasanii wenzangu tusapoti vitu vya kwenye nchi yetu, naomba tuchangie timu yetu tusisubiri kupigiwa simu, tujaribu kusapoti kwenye hili jambo. Sisi ndio tunaweza tukasimama sehemu tukawashawishi watu kufanya jambo na wakaitika,’ amesema.

Akizungumzia hali ya michango ilipofikia tangu wameanza kuchangisha Agosti 15, 2025 kupitia lipa namba, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Abdul Mashine, amesema wamekusanya sh 270, 000 kati ya milioni 73 wanazohitaji.

 “Tumeandaa lipa namba kwa ajili ya Watanzania kuchangia, lengo ilikuwa kupata watanzania milioni moja ambao kila mmoja akichangia  shilingi 100 tutakusanya shilingi milioni 100 ambazo tulitaka kuzitumia kwa timu mbili ya wanaume na wanawake. Tangu tarehe 15 tulivyoanza kukusanya hadi sasa tumefanikiwa kukusanya shilingi 270,000,”

Hata hivyo ameeleza kuwa mashindano kwa timu za wanawake yameahirishwa ambapo kwa sasa wanahitaji kiasi cha sh 73 milioni kwa ajili ya kikosi cha wanaume pekee.

Amesema Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa wamewaahidi kuwapa tiketi za ndege za kwenda na kurudi, lakini changamoto iliyopo ni kupata fedha ya mchango wa ushiriki ambayo ni Dola 4000, itayogharamia malazi na mambo mengine wakiwa nchini Burundi.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this