Arusha kupokea ugeni mkubwa, yajiandaa kufanya utalii wa mikutano

Na Mwandishi Wetu

Kitovu cha utalii na mikutano ya kimataifa nchini, Jiji la Arusha linajiandaa kupokea wageni mbalimbali na washiriki wa kikao kazi cha wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum 2025) kitakachoanza leo Agosti 23 hadi 26 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano ( AICC) jijini himo.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru amewahamasisha wageni kutumia fursa ya mkutano huo kutembelea vivutio vya kipekee vilivyopo jijini na nje ya Arusha.

“ Arusha siyo tu kitovu cha mikutano ya kimataifa bali pia ni langu Kuu la vivutio vikubwa kama Hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Manyara, Mlima Meru na Kilimanjaro, hivyo wageni wanapaswa kushuhudia uzuri wa maeneo hayo kabla ya kuondoka, “amesema Mafuru.

Ameongeza kuwa maeneo mengine ambayo Serikali inajivunia kuyatangaza ndani ya Jiji la Arusha ni makumbusho ya elimu ya viumbe hai, makumbusho ya Manifesto, chemchem ya maji ya moto na utalii wa vyakula hususani utaalamu wa kuchoma kitoweo kwenye eneo maarufu la kwa Mromboo.

Mkutano wa CEOs Forum 2025 utahusisha mamia ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo kutoa fursa ya kuonyesha urithi, vivutio na utamaduni wa Tanzania na kuimarisha diplomasia, amani na utalii.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this