
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomuza kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Kijamii (CCK), David Mwaijojele.

Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Masoud Ali Abdala (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inatarajia kufanya uteuzi Agosti 27, mwaka huu.