Doyo wa NLD achukua fomu INEC ya kuwania Urais

Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo, leo ameambatana na mgombea mwenza wake, Chausiku Khatibu Mohamed, kufika katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya kuchukua fomu za uteuzi.

Fomu hizo za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha NLD zilikabidhiwa rasmi na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu, Doyo amesisitiza dhamira yake ya kupunguza matumizi makubwa ya serikali iwapo atapewa ridhaa ya kuiongoza nchi.

Ameeleza kuwa moja ya hatua atakazochukua ni kupunguza matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi wa umma, akisema.

“Nimekuja kuchukua fomu ya uteuzi kwa kutumia bajaji leo, kama ishara ya kuwaunga mkono vijana wanaoishi maisha ya kawaida na wanaojitahidi kujikwamua kupitia kazi zao za ujasiriamali. Wastani wa maisha yao unapaswa kueleweka na kuungwa mkono na kila mmoja wetu, kuna haja ya kupunguza matumizi serikani ili tuwaunge mkono vijana wengi zaidi.”

Kwa upande wake, Mgombea Mwenza wa Urais, Chausiku Khatibu Mohamed, amewashukuru wanachama wa NLD na Watanzania kwa ujumla kwa kuonesha imani, mshikamano na moyo wa kizalendo katika kipindi muhimu cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

“Tunaamini kuwa kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko chanya kwa taifa letu, huku tukiweka msingi wa amani na mshikamano wa kweli. Amani ndiyo nguzo na tunu ya taifa letu. Chama cha NLD kimejipanga kufanya kampeni za kistaarabu, bila kudhalilisha wala kutweza utu wa mtu yeyote,” amesema.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

More like this

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...