Na Mwandishi wetu
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla amejata majina ya wagombea sita wa Jimbo Bumbuli mkoani Tanga ambapo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kipindi kilichopita Januari Makamba jina lake halijapita.
Makalla ametaja orodha ya majina ya wateule wa jimbo hilo watakaokwenda kupigiwa kura za maoni leo Julai 29,2025, jijini Dodoma, ambao ni Hidaya Kilima, Zahoro Rashid Hanuna, Eng. Ramadhan Singano, Rashid Salimu, Silas Joram na John Aloyce.
Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye atachuana na wagombea watatu ambao ni Jemedari Said, Jabiri Chilumba na Metta Nahonyo katika kulitetea Jimbo
Aidha aliyekuwa kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Matiko, amepenya katika katika kinyang’anyiro cha kura za maoni, Jimbo la Tarime Mjini mkoani Mara akiwa miongoni mwa wagombea sita walioteuliwa.