Gambo aenguliwa, CCM yateua watia nia saba kura za maoni Arusha Mjini

Na Mwandishi Wetu

KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imewateua watia nia saba kuingia katika mchakato wa kura za maoni kwa nafasi ya Ubunge wa Arusha Mjini, huku Mbunge wa sasa, Mrisho Gambo, akiwekwa kando.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 29, 2025 Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ametaja majina ya watakaopigiwa kura Agosti 4, 2025, ni Ally Babu, Hussein Gonga, Aminata Taure, Mustafa Nasoro, Paul Makonda, Rwembo Mgweno na Jasper Kishumbua.

Gambo, ambaye aliingia bungeni kwa kipindi cha kwanza kupitia jimbo hilo, hatakuwa sehemu ya mchakato huo.

Kabla ya ubunge, alihudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha, nafasi ambayo ilimuweka karibu na siasa za mkoa huo kwa muda mrefu.

spot_img

Latest articles

Watanzania Watakiwa Kujitokeza Kuomba Nafasi 1,150 za Udereva Qatar

Na Mwandishi Wetu WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya ajira iliyotangazwa na...

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

More like this