Gavana Tutuba azindua Jarida la Uchumi Wetu, Toleo Namba 1

Na Mwandishi Wetu

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba, amezindua rasmi Jarida la Uchumi Wetu, Toleo Namba 1 la Julai, 2025 linaloandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kupitia Idara ya Mawasiliano kila baada ya miezi mitatu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Jarida hilo Gavana Tutuba alipongeza kazi nzuri inayofanywa na Idara hiyo katika kuhabarisha umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania.

Ameongeza kuwa Jarida hilo litakuwa ni wenzo wa kuuwezesha umma kusoma habari zihusuzo sekta ya fedha na uchumi wa nchi kiujumla zinazotoka Benki Kuu, Serikalini pamoja na sekta binafsi.

Jarida la Uchumi Wetu limesheheni maarifa kupitia habari, makala na matukio mbalimbali na litasambazwa kwa njia ya nakala tepe (soft copies) kupitia tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania www.bot.go.tz.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this