TASAC yatoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto kusomea Ubaharia

Na Tatu Mohamed

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mohamed Salum, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwatia moyo watoto wao kuchangamkia masomo ya sekta ya bahari kutokana na uhaba mkubwa wa mabaharia nchini.

Akizungumza leo katika Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere, Salum alisema kuwa licha ya sekta hiyo kuwa na fursa nyingi za ajira, vijana wengi wanapuuza na kukimbilia taaluma nyingine.

“Sekta ya usafiri majini bado ina nafasi kubwa ya ajira, lakini vijana wamekuwa wakijikita zaidi kwenye fani nyingine. Wazazi na walezi wahamasishe watoto wao kusomea ubaharia,” alisema Salum alipokuwa akizungumza kwenye banda la TASAC.

Ameeleza kuwa ushiriki wa TASAC katika maonyesho hayo una lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya wakala huo, ikiwemo udhibiti wa usafiri majini na kuendeleza sekta hiyo kwa manufaa ya taifa.

“Ukitembelea banda letu utapata taarifa kuhusu mfuko wa mafunzo ya sekta ya bahari na fursa za masomo, zikiwemo kwa wanawake. Tunalenga kuwafikia watu wote,” alisema.

Alibainisha kuwa TASAC imekuwa ikihusika na usajili wa vyombo vya majini, kuvipa vyeti vya ubora kwa ajili ya kuendesha shughuli zake, lengo kuu likiwa ni kuhakikisha usalama na ubora wa huduma za usafiri majini.

Pia alieleza kuwa Wakala huo kupitia wataalamu wake hufanya ukaguzi wa meli za kimataifa zinazoingia nchini na kufuatilia shughuli zote katika maeneo ya baharini, ikiwemo kutoa taarifa za uokoaji, hali ya hewa, na tahadhari kwa wavuvi.

“Tunajitahidi kuhakikisha bahari inabaki safi na salama. Usalama wa bandari, utoaji wa leseni na usimamizi wa shughuli za ujenzi wa bandari ni sehemu ya majukumu yetu ya kila siku,” alisisitiza Salum.

Kwa ujumla, TASAC imeendelea kuwa miongoni mwa taasisi muhimu katika kuhakikisha usafiri wa majini unakuwa salama, unaodhibitiwa na unaowezesha fursa za kiuchumi kwa Watanzania wengi, hususani vijana.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this