Rais Samia azindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji Pamba

Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 16, 2025, amezindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji wa pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira lakini pia pamba inayozalishwa ndani ya nchi kutumika hapa nchini kuzalisha bidhaa nyingine badala ya kuisafirisha nje ya nchi kama ambavyo inavyofanyika sasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha MOLI Oil Mills Co. Ltd, Milembe Gugu Silanga kuhusu utengenezaji wa mabomba ya maji na uchakataji wa pamba kabla ya ufunguzi wa kiwanda hicho Bariadi mkoani Simiyu leo Juni 16 Juni, 2025.

“Tunajua kwamba Simiyu zao kubwa la kiuchumi ni pamba ukiacha mengine na nimshukuru mwekezaji hapa wa ndani amewaza kuongeza thamani angalau kwa hatua ya kwanza, lakini hatua ya pili sasa tutanunua kwake kuweka kwenye kiwanda ambacho tayari tumeanza kukijenga cha kutengeneza nyuzi za pamba.

“ Tunataka kusitisha kupeleka pamba yetu kama ilivyo kwenye marobota kwa wenzetu wakatengeneze nguo na watu wao wapate kazi, tunataka pamba yetu tuitengeneze hapa hapa ili watu wetu wa Simiyu waweze kupata ajira ndani ya mkoa huu,” amesema Rais Samia.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this