Kamishna wa umeme na Nishati Jadidifu afanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme Dar

▪️Aridhishwa na hatua ya utekelezaji wa miradi


▪️Awataka wakandarasi kuzingatia viwango na TANESCO kuongeza usimamizi ili kuepuka ongezeko la gharama


▪️Aisisitiza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wa uhakika

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMISHNA wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Juni 12, 2025, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme ya Gridi Imara inayoendelea katika Jiji la Dar es Salaam, na kutoa maelekezo muhimu kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo.

Miradi hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha huduma bora na ya uhakika kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Kamishna amesema ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo, licha ya changamoto mbalimbali za kimazingira, na kusisitiza umuhimu wa kuendelea na jitihada za kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

“Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa, lakini nimeagiza wakandarasi waharakishe kazi, vifaa vipatikane kwa wakati, na viwango vya kazi vizingatiwe ili miradi hii itoe matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi,” amesisitiza Mhandisi Luoga.

Akifafanua amebainisha kuwa miradi hiyo ya kimkakati, inayotekelezwa na TANESCO kwa ufadhili wa Serikali, inalenga kuboresha huduma ya umeme kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini.

Aidha, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuidhinisha rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo muhimu.

Katika maagizo yake, ameitaka TANESCO kuongeza usimamizi kwa wakandarasi katika kuhakikisha upatikanaji wa vifaa kwa wakati, na kusimamia ubora wa kazi ili kuepuka ongezeko la gharama zitokanazo na ucheleweshaji.

Kwa upande wake, Mhandisi Abdallah Chikoyo, Meneja wa Miradi ya Kuzalisha Umeme TANESCO aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji , ameahidi kuongeza juhudi katika usimamizi wa miradi na kuweka mipango kazi inayotekelezeka kwa wakati.

“Tumejipanga kuongeza nguvu katika usimamizi wa miradi hii, na kuimarisha ushirikiano na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ufanisi, tukitimiza wajibu wetu katika kuboresha huduma ya umeme nchini,” amesema Mhandisi Chikoyo.

Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Serikali katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo Kamishna Luoga alitembelea vituo vya umeme vya Ubungo I, Mabibo, Kinyerezi na Gongo la Mboto.

Katika vituo hivyo, kazi ya ufungaji wa mashine umba zenye uwezo mkubwa (transformers) inaendelea kwa kasi ya kuridhisha, ikiwa ni hatua ya kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme jijini Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU

📌Waziri Ndejembi ashuhudia utiaji saini, asema ni alama ya miradi ya kielelezo nchini 📌Mradi utakuwa...

NDEJEMBI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA SHILINGI BILIONI 204.7 WA MRADI WA UMEME WA JUA WA MEGAWATI 100 KISHAPU

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi, leo Julai 27, 2026, ameshuhudia...

DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA

Na Mwandishi Wetu KUFUATIA kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini...

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

More like this

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU

📌Waziri Ndejembi ashuhudia utiaji saini, asema ni alama ya miradi ya kielelezo nchini 📌Mradi utakuwa...

NDEJEMBI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA SHILINGI BILIONI 204.7 WA MRADI WA UMEME WA JUA WA MEGAWATI 100 KISHAPU

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi, leo Julai 27, 2026, ameshuhudia...

DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA

Na Mwandishi Wetu KUFUATIA kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini...