Ndege ya Air India yaanguka, ikiwa na abiria  242

Na Mwandishi Wetu

Ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la  India ‘Air India’  iliyokuwa inatokea nchini India kwenda London nchini Uingereza imeanguka na kuwaka moto leo Juni 12, 2025 katika eneo la Ahmedabad India muda mfupi baada ya kupaa ikiwa na watu 242.

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka nchini India zimesema ndege hiyo ilikuwa imebeba  abiria 169 ni raia wa India,  raia wa  53 Uingereza, Wareno saba na raia wa Canada mmoja, huku wafanyakazi wa ndege hiyo  ni 12.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi  kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, amesema ameshtushwa sana na ajali hiyo ya ndege.

“Ajali ya Ahmedabad imetushtua na kutuhuzunisha. Haielezeki jinsi inavyovunja moyo, amesema Modi katika ujumbe huo alioandika.

Mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa Flightradar24 umesema ndege hiyo ilikuwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, mojawapo ya ndege za kisasa zaidi zinazotumika.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this