Wasira: Hatuahirishi Uchaguzi Mkuu ng’o

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitaahirisha uchaguzi ng’o kwa sababu kiliomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano na kimeongoza vizuri kwa kuleta maendeleo chini ya serikali iliyoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akiwasalimia wanachama, wapenzi wa Chama na wananchi waliofika ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma kumlaki akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

“Tuliomba ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa miaka mitano, tumeiongoza Tanzania, tumefanya kazi yetu vizuri halafu unatuambia tuahirishe, ahirisha wewe mambo yako sisi hatuwezi ng’o, sisi tunagombea, tumeshaweka wagombea, tumemuweka Daktari Samia Suluhu Hassan (mgombea urais kupitia CCM), tumemuweka Dk. Emmanuel Nchimbi (Mgombea Mwenza wa CCM).

“Sasa wako rafiki zangu wale wa ‘tone tone’ wao wanapita wanawaambia tusifanye uchaguzi na mimi nawauliza tukiacha kufanya uchaguzi nchi itakuwa inaongozwa na nani, maana huwezi kuwaambia watu acheni uchaguzi halafu huwapi mbadala eti tuahirishe, tuahirishe nini?,” alieleza na kuhoji.

Alisema kuwa kote ambako wamepita na hata ambako bado hawajapita, CCM iko imara na inamuunga mkono Dk. Samia Suluhu Hassan na hawamuungi kwa sababu zozote ambazo hazielezeki, bali wanamuunga kwa sababu ya maendeleo makubwa aliyoyafanya “haya mnayoyasikia ameyafanya Songea ndiyo hayo hayo ameyafanya Tanzania nzima,”.

spot_img

Latest articles

Ajali ya moto yaua watoto yatima watano

Na Mwandishi Wetu Watoto watano waliokuwa wanalelewa katika kituo cha watoto yatima cha Igambilo Manispaa...

Januari Makamba hayumo, Nape apeta uteuzi CCM

Na Mwandishi wetu Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Rais wa Yanga akatwa uteuzi Jimbo la Kigamboni, Jemedali, Shafii Dauda mambo mazuri

Na Mwandishi Wetu Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Saidi ameshindwa kupenya katika  uteuzi...

CCM yamtema Luhaga Mpina

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, hatakuwa miongoni mwa wanaowania ubunge kupitia...

More like this