Msajili hazina aongoza mazungumzo ya uwekezaji na kampuni ya Uswisi

Na Mwandishi Wetu, Abidjan

MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, Mei 14, 2025, ameongoza mazungumzo ya kitaalamu kati ya Serikali ya Tanzania na Soren Toft, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mediterranean Shipping Company (MSC), kuhusu uwekezaji wa kimkakati katika Bandari ya Dar es Salaam na Mangapwani–Zanzibar.

Mazungumzo hayo na kampuni ambayo makao yake makuu yapo Geneva, Uswisi, yamefanyika jijini Abidjan, Côte d’Ivoire pembezoni mwa Jukwaa la Maafisa Watendaji Wakuu Afrika, yakilenga fursa za kuboresha huduma na miundombinu ya bandari hizo mbili muhimu kwa uchumi wa taifa na ukanda wa Afrika Mashariki.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kupitia kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Pascal Maganga, kimeihakikishia MSC kuwa kipo tayari kushirikiana kikamilifu kwa kuhakikisha mazingira rafiki ya uwekezaji ili uwekezaji huo ufanyike kwa mafanikio makubwa.

Kwa upande wake, Toft ameonyesha dhamira ya dhati ya MSC kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha miundombinu ya bandari, akisisitiza umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam na Mangapwani kama lango kuu la biashara kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Tanzania inaendelea kujidhihirisha kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika, kwa kushirikiana na wadau wakubwa wa kimataifa katika kuendeleza miradi ya kimkakati itakayochochea uchumi wa nchi na ajira kwa wananchi.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

Hizi ndizo hisia dhidi ya INEC, Msajili wa Vyama vya Siasa

KATIKA safu hii wiki iliyopita niliandika uchambuzi nikihoji, ‘INEC, Msajili wa Vyama wanaweza kutupa...

More like this