Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameiwezesha Simba katika safari kwenda Afrika Kusini kwa kugharamia usafiri na malazi kwa timu hiyo katika kipindi chote itakapokuwa huko kwa ajili ya mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch, Aprili 27, 2025.
Simba ambayo imeondoka leo, katika mchezo wa kwanza uliopigwa M kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji amemshukuru Rais Samia kwa sapoti hiyo, huku akisema klabu hiyo inatambua juhudi za Rais katika kuimarisha michezo.
“Kwa niaba ya Klabu ya Simba Sports Club, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha klabu yetu kushiriki mashindano ya kimataifa.
“Tumepokea kwa moyo wa shukrani mchango wa malazi na usafiri kwa ajili ya mchezo wetu wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaofanyika Afrika Kusini.