Lissu afikishwa mahakamani Kisutu, asomewa shtaka la uhaini na kuchapisha taarifa za uongo

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la uhaini pamoja na kuchapisha taarifa za uongo kwa lengo la kupotosha umma.

Lissu amefikishwa mahakamani hapo leo Aprili 10, 2025 saa 10: 15, huku Wakili Nassoro Katuga akimsomea shitaka hilo.Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dkt. Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mwanasiasa huyo alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.

Lissu amesomewa kesi ya uhaini chini ya kifungu cha sheria cha 39(2) cha kanuni ya adhabu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga na wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga.Inadaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam.

Katuga amedai kuwa siku ya tukio mshtakiwa Lissu akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam alitangeneza nia ya kushawishi au kuchochea umma ya kuweza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa kusema maneno yafuatayo.

“Walisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi, hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko….kwahiyo tunaenda kukinukisha sanasana huu uchaguzi tutaenda kuvuruga kwelikweli, tunaenda kukinukisha vibaya sana”.

Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhaini ambazo kwa kawaida husikilizwa Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na wameomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wa Utetezi, Dkt. Nshala Rugemereza ulidai sheria inasema mtu afikishwe mahakamani upelelezi ukiwa umekamilika, lakini wanashangaa mteja wao amefikishwa mahakamani na wanaambiwa upelelezi bado.

“Ibara ya 14 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya mtu kuwa uhuru lakini inaonyesha upande wa mashtaka wana nia ovu kwani wanamkamataje mtu upelelezi ukiwa bado?.

“Tunaomba ama kesi ije kwa ajili ya kusikilizwa au mteja wetu aachiwe huru au apelekwe mahakamani pale upelelezi utakapokuwa umekamilika,” alidai.

Wakijibu hoja hiyo, Wakili Katuga alidai kuwa ni kweli sheria inataka mtu kufikishwa mahakamani upelelezi ukiwa umekamilika lakini kuna kesi ambazo zinaweza kufikishwa mahakamani kutokana na usiriasi wake kama ilivyo kesi hiyo.

Hakimu Kiswaga alikuballiana na hoja za upande wa mashtaka na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 24, 2025.

Kesi ya pili, inayohusu mashtaka ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni imesomwa na wakili wa serikali Harrison Lukosi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini.

Imedaiwa Aprili 3, mwaka huu jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulangai umma alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka ‘ Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana , wagombea wa Chadema walienguliwa kwa melekezo ya Rais.

Maneno mengine yalisomeka ‘ Mapolisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi, pia alichapisha maneno yaliyosomeka Majaji ni Ma-CCM hawawezi kutenda haki wanapenda wapate teuzi kuchaguliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa’.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi umekamilika hiyo Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Aprili 24 mwaka huu Lissu atakaposomewa hoja za awali.

Katik kesi hii, Lissu aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya sh milioni tano na kitambulisho cha Nida.Mwisho

spot_img

Latest articles

Waogeleaji wa Lake Victoria Sports Club waahidi kuing’arisha Tanzania Kimataifa

Na Mwandishi Wetu Jumla ya waogeleaji sita  chipukizi wa Lake Victoria Sports Club  ya jijini...

Mbunge Kimei kinara kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa...

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...

Kafulila: Hatuwezi kujenga uchumi wa nchi bila kushirikisha sekta binafsi

Na Tatu Mohamed, Mwanza MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma...

More like this

Waogeleaji wa Lake Victoria Sports Club waahidi kuing’arisha Tanzania Kimataifa

Na Mwandishi Wetu Jumla ya waogeleaji sita  chipukizi wa Lake Victoria Sports Club  ya jijini...

Mbunge Kimei kinara kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa...

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...