HDT yaja na SeamossPlus kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kukabiliana na changamoto ya magonjwa yasiyoambukiza(NCDs), Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Health Promotion Tanzania (HDT) imekuja na kifurushi cha virutubishi kinachoitwa SeamossPlus ili kupambana na magonjwa hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu virutubishi hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HDT, Dkt. Peter Bujari amesema vinafanya kazi mwilini ndani ya wiki moja.

Amefafanua kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za Mwaka 2021 zinaonesha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza imeongeza na kufikia asilimia 38.8 kutoka asilimia 34 kwa mwaka 2019.

Ameongeza kuwa wanaume 557 na wanawake 498 kwa kila 100,000 wanapoteza maisha kwa mwaka kutokana na magonjwa hayo.

“Kutokana na takwimu hizi, inaonyesha kuwa hatari ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu, moyo na saratani yanaongezeka na vifo pia vinaongezeka. Na ikiendelea hivi kwa miaka mitano ijayo vifo vinaweza kufikia hata asilimia 40 kama hatua hazijachukuliwa.

“Magonjwa yasiyoambukiza yanaepukika kwasababu yanatoka na mtindo wa maisha, kwahiyo HDT kwa kuliona hili, tukaona tuje na bidhaa hii ya SeamossPlus ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na magonjwa yasiyoambukiza,” amesema.

Amebainisha kuwa SeasmossPlus imetengenezwa kwa Mwani na kuchanganywa na Tangawizi, kitunguu swaumu, Bibo, Alovera na mchaichai.

“SeamossPlus inaondoa sumu mwilini, Ina Omega 3 na 6 ambayo huzuia utengenezwaji wa seli za saratani na hupunguza Cholesterol mbaya…pia huzuia uharibifu wa seli unaosababishwa na saratani, kuzeeka haraka na hupunguza tindikali mwilini ambayo husababisha hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza,” amesema.

spot_img

Latest articles

Kapinga azindua Kituo Mama cha gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) DAR

📌 Ni cha Pili kwa ukubwa barani Afrika, Cha Kwanza kwa ukubwa EAC 📌 Kujaza...

Mapato yasiyo ya kodi yafikia asilimia 67, OMH yadhamiria kufikia lengo la mwaka

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imeendelea kuonesha mafanikio...

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...

More like this