PURA kunadi vitalu 26 vya utafutaji mafuta na gesi asilia

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inatarajia kunadi vitalu 26 vya gesi asilia na mafuta kwa lengo la kuvutia wawekezaji ili kuchangia maendeleo na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam Machi 5, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la 11 na Maonesho ya Petroli nchi Wanachama Afrika Mashariki (EAPCE’25).

Sangweni amesema kuwa kati ya vitalu 26 vitakavyonadiwa, 23 vinapatikana katika Bahari ya Hindi, huku vitatu vikiwa katika Ziwa Tanganyika. Ameeleza kuwa kutokana na ugunduzi wa gesi katika maeneo hayo, kazi inaendelea ya kuzihakiki.

“Mpango wa Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuweka nguvu zaidi katika suala la utafutaji wa mafuta na gesi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inahamasisha nishati safi ya kupikia,” amesema Sangweni.

Amesisitiza kuwa mwaka huu kwao ni muhimu kwani kati ya shughuli wanazofanya ni kunadi na kuhamasisha uwekezaji katika tasnia ya utafutaji wa mafuta na gesi na kwa kuanzia PURA tayari wana maeneo hayo ambayo wameyawekea mipaka ili waweze kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza na kuanza shughuli hizo hapa nchini.

Aidha amesema kama watu wanavyofahamu Tanzania imegundua gesi kiasi cha futi za ujazo Trilioni 57.54 na kwamba gesi iliyogundulika kuna uhakika wa kupata soko hapa nchini na masoko ya nje kama Japan, Korea na nchi nyinginezo.

spot_img

Latest articles

NEMC yatoa elimu kwa umma kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Na Tatu Mohamed BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza kutoa...

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Naibu Waziri wa Nishati akabidhi vitendea kazi Kwa Tanesco Mkoa wa Shinyanga

📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi 📌Awasihi wananchi kutumia...

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....

More like this