Wafanyakazi Jiji la Dar kizmbani kwa kusababisha hasara ya Bilioni 8

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakituhumiwa kwa makosa 143 likiwemo la kuisababishia halmshauri hiyo hasara ya Sh bilioni 8.9.

Wafanyakazi hao ni Afisa Mtendaji wa Kata, Khalid Nyakamande (34), Afisa Afya Patrick Chibwana (40), Karani wa Fedha, Judica Ngowo (51), Tulusubya Kamalamo (53), James Bangu (57) na Mohamed Khais (41).

Wengine ni Abdallah Mlwale (52), Deogratias Lutaza (55), Febronia Nangwa (44), Grory Eugen (46), Said Bakari (37), Josephine Sandewe (48), Dorica Gwichala (45), Jesca Lugonzibwa (53) na Ally Baruani (38) wote wakazi wa Dar es Salaam.

Akisoma hati ya mashitaka Juni 26, 2023, Wakili wa Serikali Faraji Ngukah akisaidiana na Pendo Temu amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo wa Mahakama hiyo kuwa washitakiwa wanatuhumiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka 143, ambapo waliyatenda kati ya Julai Mosi, 2019 na Juni 30,2021.

Amedai kuwa mashitaka hayo kuongoza genge la uhalifu, matumizi mabaya ya madaraka, kuingiza taarifa za uongo kwenye mfumo, ufujaji na ubadhirifu, kughushi, utakatishaji fedha na kusababishia hasara.

Ngukah amedai kuwa washitakiwa wanatuhumiwa kuongoza genge la uharifu, na kusababisha kujipatia Sh bilioni 8.9, ambapo walitenda kosa hilo kati ya Julai Mosi, 2019 na Juni 30,2021.

Amedaiidai kuwa katika, shitaka la matumizi ya madaraka washitakiwa wote 15 wakiwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa nyadhiwa mbalimbali walishindwa kuingiza mapato katika akaunti ya NMB, CRDB, NBC na DCB zinazomilikiwa na jiji na kusababisha hasara ya Sh 8,931,598,500.

Katika shitaka la kuingiza taarifa za udanganyifu kwenye mfumo, Ngukah alidai kuwa shitaka hilo linamkabili Ngowo, Nangwa na Bakari, ambapo wanatuhumiwa kulitenda kati ya Julai Mosi, 2019 na Juni 30,2021.

Wakili huyo aliendelea kudai kuwa katika shitaka la ufujaji na ubadhilifu linawakabili Kamalamo, Bangu, Khais, Mlwale, Lutaza, Ngowo, Nangwa, Eugen, Bakari, Sandewa na Lugonzibwa ambapo wanatuhumiwa kutumia fedha za halmashauri hiyo kwa maslahi yao binafsi.

Ngukah amedai kuwa katika shitaka la kughushi linamkabili Kamalamo, Bangu, Sandewa, Gwichala, Lugonzibwa, Chibwana, Baruani na Nyakamande.

Amedai kuwa katika shitala la utakatishaji fedha, washitakiwa wanatuhumiwa kutenda kosa hilo Julai Mosi, 2019 wakiwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wanatuhumiwa kuisababishia hasara mamlaka husika Sh bilioni 8.9.

Baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka hayo, hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, ambapo Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka.

Wakili Ngukah, amedai upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kwa kesi hiyo, ambapo Mahakama imepanga Julai 10, mwaka huu kwa kutajwa.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...