Na Mwandishi Wetu
Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya) imeendelea kujinasua katika nafasi za chini baada ya leo Februari 15, 2025 kuichapa Coastal Union mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa dimba la CCM Kirumba, Mwanza.
Matokeo hayo yanaifanya Pamba kufikisha alama 21 katika michezo 19, ikipanda hadi nafasi ya nane kutoka ya 13 . Huo ni mchezo wa tatu mfululizo kushinda, mechi iliyopita iliifunga Azam FC 1-0 kwenye uwanja huo, kabla ya hapo ilitoka kuipiga Dodoma Jiji 1-0 ugenini.